EPL

Ronaldinho: Natamani ningecheza na Mo Salah!

Sambaza....

Nguli wa Timu ya Taifa ya Brazil “selecao” na klabu ya Barcelona Ronaldinho Gaucho ameshindwa kuficha hisia zake juu ya kiwango cha nyota wa Liverpool na Timu ya Taifa ya Misri Mohamed Salah.

Ronaldinho akizungumza akiwa nchini Misri na Kingofoot.com amesema Salah ni miongoni mwa nyota wenye vipaji vikubwa na angetamani kucheza pembeni yake.

Ronaldinho Gaucho.

“Nilitamani ningecheza pamoja na Mohamed Salah. Yeye ni mmoja wa wachezaji bora duniani ambao huwa napenda kuwatazama,” Ronaldinho 

Gaucho mshindi wa Ballon’dor pia hakusita kutoa ushauri wa wapi anadhani Mo Salah anatakiwa kwenda huku akisisitiza furaha ni muhimu kwake katika mchezo wa soka.

Mohamed Salah

“Ushauri kwa Salah kuhusu mustakabali wake? Muhimu zaidi ni yeye kuwa na furaha, soka ni chanzo cha furaha na lazima iwe haijalishi anachezea klabu gani hapo baadaye.” Alisema Gaucho

Mo Salah baada ya kuibuka mfungaji bora wa EPL sasa anajiandaa na fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid itakayopigwa Jumamosi hii.

Sambaza....