Aishi Manula "Air Manula"
Stori

Simba Bila Manula? Ngoja Tuone

Sambaza....

Wapwa, Aishi Manula anakaa nje kwa muda mrefu, Je nani anayeziba nafasi yake kwa muda ambao atakuwa nje ya Uwanja?

Rahisi, hapa Simba SC ilikuwa lazima watafute golikipa mwingine ambaye atakuja kuongeza nguvu pamoja na Ally Salim katika eneo hilo ambalo pia yupo Ahmad Feruz ambaye  hana uzoefu mkubwa.

Feruz na Salim wote ni Magolikipa ambao hawajapata dakika nyingi sana za kucheza pale Simba hata nsimu uliomalizika uwepo wa Aishi Manula na Beno Kakolanya pale naona ilikuwa ni sehemu ya wao kupata darasa.

Ally Salim.

Ni ngumu sana Simba kwenda kuanza mashindano bila Aishi Manula na Beno Kakolanya ambaye tayari kaondoka jumla. Hii ilikuwa karata ngumu sana kwa Simba kuicheza kwenye eneo hilo.

Jefferson Luis anaingia ndani ya Simba na moja kwa moja ndiye mbadala wa Aishi Manula labda mpaka atakaporudi. Maswali ni mengi kwa watu mbele ya Jefferson, Je ataweza kufanya alichokuwa anafanya Aishi Manula ?

Sifahamu vizuri kuhusu yeye kwenye eneo la golini tofauti na kuona mtandaoni ila kwa mazingira anayotoka na timu alizocheza kwa muda mfupi huenda akaongeza kitu ndani ya Simba. Klabu haiwezi kwenda nje kufata mtu ambaye hawakuwahi kumfuatilia

Jefferson Luis.

Jefferson Luis kuanzia mwaka 2017 amecheza soka katika Klabu 6 za zote zinatoka nchini Brazil ( Resende, Athletic, Itabaiana, Volta Redonda, SC Aymorés na Itabirito FC ambapo mkataba wake umemalizika 2023.

Hii ilikuwa lazima ifanyike tena kwa uharaka mkubwa. Ally Salim na Feruz ilikuwa karata ngumu sana kwa Simba SC kuicheza kuelekea Msimu mpya wa mashindano.

Muda utaongea tusubiri kuona Jefferson Luis ataongeza kitu gani ndani ya Timu kwenye Eneo hilo ambalo ni nyeti sana katika Mpira wa Miguu.


Sambaza....