Jezi watakazotumia Simba katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika
Mabingwa Afrika

Simba katika mstari mwembamba wa kifo na uhai!

Sambaza....

Kikosi cha Simba jioni ya leo kitakua katika Dimba la St Marys pale Entebe Uganda kwenda kufahamu hatma yao ya ushiriki wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa msimu huu.

Simba ipo Kundi C ikiwa na alama sifuri wakishika mkia katika kundi ambalo linaongozwa na Raja Casblanca wenye alama sita, Horoya wana alama nne halafu kuna huyu Vipers mpinzani wa Simba mwenye alama moja.

Simba ilianzia ugenini nchini Guinea wakafungwa bao moja kwa sifuri, wakati huo Raja akampa bao tano Vipers. Mchezo wa pili Simba akafa tatu bila Kwa Mkapa mbele ya Raja, upande wa pili Vipers na Horoya wakatoka suluhu. Maana yake katika kundi hilo vibonde ni Simba na Vipers.

Mchezo wa leo kwa Simba una maana kubwa mno na ndio uliobeba hatma yao kama wataendelea kushiriki tu ili kukamilisha ratiba ama watafufua matumaini yakufuzu robo fainali.

Licha yakupoteza michezo yote miwili lakini bado Simba wananafasi yakufuzu kwenda robo fainali endapo watafanikiwa kupata alama tisa au kumi na mbili kwa kushinda michezo mitatu ama yote iliyosalia huku wao wakimuombea mabaya Horoya mbele ya Raja Casablanca.

Simba wanahitaji kwa hali na mali alama sita za Vipers na ili zipatikane zote wanapaswa kwanza kuanza kuvunja ngome pale Entebe na kubeba alama tatu mbele ya Vipers katika Dimba lao la St Mary.

Kama Simba wakifanikiwa kupata alama tatu katika mchezo wa leo maana yake watakua wanasubiri kupata alama tatu nyumbani tena dhidi ya Vipers halafu wakiwasubiri Horoya kwa Mkapa ambae ndie atakua mshindani mkubwa katika kundi nyuma ya Raja ambae ana nafasi kubwa yakuongoza kundi.

Mzamiru Yasin (katikati) akiwatambuka wachezaji wa Raja Casablanca.

Lakini endapo Simba watapata sare ama kupoteza maana yake ndoto zao zakufika nusu fainali mwaka huu zitakua zimekufa rasmi bila kujali matokea ya Horoya dhidi ya Raja.

Simba inapaswa kubadilika na kupandisha morali yao na kuachana na fikra zakutokupata matokea katika michezo mitatu mfululizo. Wachezaji ni lazima waamke warudi katika ari yao ya upambanaji ili kuifunga Vipers na kuamsha matumaini yao.

Huenda kikosi kikaanza hivi!

1. Manula
2. Kapombe
3. Tshabalala
4. Onyango
5. Inonga
6. Kanoute
7. Chama
8. Mzamiru
9. Baleke
10. Phiri
11. Sakho

Sub: Kakolanya, Mwenda, Kenedy, Sawadogo, Kibu, Saidoo, Banda, Bocco

Sambaza....