Mlinzi huyo wa kati alikuwepo wakati Simba inafuzu robo fainali mbele ya AS Vita katika msimu wa mwaka 2019 kabla yakutolewa na TP Mazembe robo fainali.
Simba wanakwenda kutupa karata yao ya nne katika kundi lao ambapo msimamo wa kundi unaonyesha bado wana nafasi wakiwa na alama zao tatu huku wapinzani wao Vipers wakiwa na alama moja pekee.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo Raja Casablanca atamkaribisha Horoya kutoka Guinea katika dimba la Mohamed VI mabapo Vipers alisuulubiwa kwa mabao matano kwa sifuri.
Lakini endapo Simba watapata sare ama kupoteza maana yake ndoto zao zakufika nusu fainali mwaka huu zitakua zimekufa rasmi bila kujali matokea ya Horoya dhidi ya Raja.
Simba si tu hawana alama lakini pia hawajafunga bao lolote mpaka sasa katika michuano hiyo hivyo mchezo wa Vipers unatarajiwa kuwa mgumu na wakufufua matumaini yao yakufuzu robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika.