Ligi Kuu

Simba ngoma ngumu, Yanga wapasuka

Sambaza....

Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite imeendelea leo kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali huku wababe Simba Queens na Yanga Princess wakikosa matokeo mazuri.

JKT Queens walikua wenyeji wa Simba wakiwa uwanjani kwao Isamuhyo Mbweni na kufanikiwa kupata sare ya bao moja kwa moja na hivyo kufanikiwa kupata alama nne kwa Simba Queens msimu huu.

 

JKT ndio walikua wakwanza kupata bao ambapo katika dakika ya 43 kupitia kwa fauli iliyopigwa na Deonisia Minja na kuingia moja kwa moja. Simba walifanikiwa kusawazisha kupitia kupitia kwa Jentrix Shikangwa katika dakika ya 52 baada yakupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango.

Yanga wao walikua ugenini katika Dimba la Jamuhuri Morogoro wakiwa wageni wa Fountaine Gate Princess na kukubali kichapo cha bao moja kwa bila kama walivyokutana mchezo wa raundi  ya kwanza.

Kwa matokeo hayo sasa Simba Queens wanafikisha alama 23 sawa na Fountaine Gate Princess wakifungana kileleni. JKT Queens wameshuka mpaka nafasi ya tatu huku Yanga wakiendelea kubaki nafasi ya nne.

Matokeo mengine Baobab Queens wameifunga Amani Queens bao tatu bila. Ceassia Queens wameibuka na ushindi wa mabao manne kwa matatu dhidi ya Alliance Queens. Mkwawa Queens wamepoteza nyumbani kwa bao moja bila mbele ya Tiger Queens.

Sambaza....