Saidoo Ntibazonkiza akipiga shuti mbele ya walinzi wa Vipers
Stori

Simba yamfukuzisha kocha.

Sambaza....

Wababe wa Uganda Vipers Fc imekubaliana kuachana na kocha wake kutokana na matokeo yasiyoridhisha tangu apate kibarua hicho baada ya miezi miwili akiwa kazini.

Vipers kupitia tovuti ya klabu imethibitisha kuachana na kocha Beto Biachi mara baada ya kocha huyo kupoteza mbele ya Simba na hivyo kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

“Vipers Sports Club inatangaza kuwa kandarasi ya kocha mkuu Beto Bianchi imesitishwa mara moja,” taarifa ilisema.

“Klabu ingependa kumshukuru kwa juhudi zake za kutochoka wakati alipokua klabuni na kumtakia mafanikio katika majukumu yake ya baadae,” taarifa iliongeza.

Beto Bianchi alichukua nafasi ya Robertinho Oliveira aliyejiunga na Simba baada ya kuwatoa TP Mazembe na kuwapeleka hatua ya makundi. 

Bianchi ameiongoza Vipers katika michezo sita akiwa hajapata ushindi hata mchezo mmoja wala kufunga hata bao moja. Amefungwa mitatu na sare tatu.

Sambaza....