Stori

Maswali Magumu Yanayohitaji Majibu Cairo!

Sambaza....

Mashindano ya African Football League yanaendelea baada ya mchezo wa ufunguzi kati ya Simba na Al ahly kumalizika kwa sare ya magoli mawili kwa mawili katika dimba la Mkapa jijini Dar es salaam (Tanzania).

Mchezo huo uliopigwa juzi tarehe 20, Al Ahly alikuwa ugenini huku Simba wakiwa nyumbani, kulipigwa mpira mwingi sana licha ya timu zote kutoshana nguvu.

Ahly walikuwa wakwanza kupata goli mapema kipindi cha kwanza kabla ya Simba kuchomoa kipindi cha pili dakika za mwanzoni kupitia Kibu Denis kwa mpira wa kichwa kisha badae kidogo dakika ya sitini Sadio Kanoute aliwapa Simba bao la uongozi kwa kichwa kikali lakini dakika tatu badae Mohamed Kakhraba alichomoa na kuufanya ubao usomeke mbili mbili mpaka dakika ya mwisho.

Sadio Kanoute akifunga bao la pili la Simba katika mchezo huo.

Ahly alitengeneza nafasi nyingi hususani katika kipindi cha kwanza cha mchezo licha ya kuzitumia kwa ufinyu alistahili kuibuka na ushindi, lakini Simba pia alistahili ushindi kwani aliutawala mchezo kwa dakika 45 zote za kipindi cha pili.

Mechi ya marudiano ya mchezo huu ambao mshindi wa jumla atakwenda nusu fainali utachezwa Jumanne ya tarehe 24 mwezi huu jijini Cairo. Inafahamika Al Ahly akiwa nyumbani anakuwa mgumu sana kufungika ingawa lolote linaweza kutokea.

Waneni husema mfupa uliomshinda fisi ukimpa mbwa utamuua, lakini huyu ni Simba sio mbwa anaweza uvunja mfupa huo haijalishi ni mgumu kiasi gani.
Al ahly waliomba Shirikisho la soka la nchini Misri kuwaruhusu kuujaza uwanja yaani “fullhouse” ukizingatia kwamba wamepewa ruhusa ya mashabiki elfu 30 pekee.

Clatous Chama akimuacha kiungo Aliou Dieng wa Al Ahly.

Kwa mujibu wa Al Ahly wenyewe wamesema mapato ya mchezo huo watapatiwa wahanga wa Palestina katika vita dhidi ya Israel.

Je Simba ataweza kumzuia Al Ahly? Atawezaje kuibuka na ushindi katika dimba la Cairo International ambalo ni gumu sana kwa timu wageni? Je Simba atazimudu kelele za mashabiki elfu 75 kwa dakika zote 90? Unafikiri Simba wachezeje ili wapate ushindi? Kikosi je?

Basi usijali Kandanda.co.tz iko hapaa kwa ajili yako, Kandanda.co.tz iko hapa kukupa majibu yote. Tukutane hapa chini katika maoni. Hadi wakati mwingine kwaheri!!!

Sambaza....
Subscribe
Notify of

1 Gumzo
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
1
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x