Zamani

Unakumbuka Kali ya Zidane Pale Ujerumani?

Sambaza....

Tarehe kama ya Leo miaka 17 iliyopita Zinedine Zidane ‘Zizou’ alimaliza maisha yake ya soka la Kimataifa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa Marco Materazzi kwenye fainali ya kombe la Dunia mwaka 2006.

Tukio hilo lilikuwa gumzo dunia nzima ambapo baadhi ya watu wanasema inawezekana ile kadi nyekundu ndio ulichafua sifa yake na kushindwa kutwaa tuzo ya Uchezaji bora wa mashindano na mchezaji bora wa dunia kwa ujumla.

Zinedine Zidane akimtwika kichwa Marco Materazi.

Zinedine Zidane Yazid maarufu kama Zizzou alikuwa na kiwango bora kwenye michuano hiyo ya kombe la Dunia 2006 nchini Ujerumani na kuipelekea Ufaransa fainali.

Ufaransa ikapoteza fainali hiyo mbele ya Italia kwa mikwaju ya penati ambapo mambo yalikua hivi.

Matokea ya Fainali ya Kombe la Dunia 2006
ITALY 🇮🇹 1-1 FRANCE 🇫🇷
⚽️ 19″Materazzi ⚽️ 7″ Zidane (p)

Mikwaju ya matuta,
ITALY 🇮🇹 5️⃣-3️⃣ FRANCE 🇫🇷

✅️ Pirlo           ✅️ Gallas
✅️ Materazzi  ❎️️ Trezeguet
✅️ De Rossi     ✅️ Abidal
✅️ Del Piero    ✅️ Sagnol
✅️ Grosso

Abuu Mwakyoma

Sambaza....