Pamba Sc
Zamani

Unaikumbuka hii Pamba Sc!?

Sambaza....

Hawa ndio Wana TP Lindanda wapinzani wakubwa wa “Wanakishamapanga” Toto Africans pale Jijini Mwanza, ni kama upinzani uliopo kati ya Coastal Union na African Sports pale Tanga ama Simba na Yanga.

Pamba hii ndio ilikua ikikukuta uwanjani kizembe inakupigia kandanda la hali ya juu na magoli yakutosha na kupelekea kuwa tishio mnoo kwenye miaka ya tisini. 

Pamba Sc.

Hapo juu ni kikosi cha zamani cha Pamba ya Mwanza. Waliosimama Kutoka (kushoto) ni Golikipa Madatta Lubigisa, Rajab Msoma (RIP), Beya Simba, Nteze John Lungu, Kitwana Selemani, Fumo Felician, Pascal Mayalla na Golikipa Paul Rwechungura. Kutoka (Kushoto) Waliokaa ni George Gole, Khalfan Ngassa “Babu”, Ally Bushiri, Alphonce Modest, Mao Mkami “Ball Dancer”, Saleh Mohamed, Hamisi Nyembo na Nicodemus Bambaga(RIP).

Tuambie unaikimbuka kwa lipi Pamba hii ambayo ilikua mwiba katika miaka ya tisini haswa katika Dimba la CCM Kirumba pale Mwanza!?


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.