Sambaza....

Manchester United imepata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stoke City, katika mchezo wa ligi kuu ya soka Uingereza maarufu kama EPL

Katika mchezo huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo kunako dimba Old Trafford, Manchester United walipata bao la uongozi mapema dakika ya 9 kupitia kwa Antonio Valencia akimalizia kazi ya kiungo Paul Pogba

Dakika ya 38, Antonio Martial aliipatia United bao la pili akimalizia kazi ya Paul Pogba, na kufanya hadi timu zinakwena mapumziko United wakiwa mbele kwa mabao hayo mawili

Stoke midfielder Ireland got his shot away but it drifted wide of David de Gea's right post, much to the relief of the United fans

Kipindi cha pili United waliendelea kulisakama lango la wapinzani wao, na jitihada zao kuzaa matunda kunako dakika ya 72, kufuatia mshambuliaji Romelu Lukaku kuukwamisha mpira wavuni na kuhitimisha ushindi huo wa mabao 3-0

Kwa ushindi huo United sasa imefikisha alama 50, ikizidiwa kwa alama 12, na vinara wa ligi hiyo Manchester City

United iliwakilishwa na; David De Gea, Antonio Valencia, Luke Shaw, Phil Jones, Criss Smalling, Nemanja Matic, Juan Mata/Scott Mctomnay dk 83, Paul Pogba, Antonio Martial/ Marcus Rashford dk 80, Jesse Lingard / Maroane Fallaini na Romelu Lukaku

Stoke city; Jack Butrand, Maritz Bauer, Josh Tymon/ Kevin Summer dk 46, Kurt Zouma, Bruno India, Darren Fletcher, X Shaqir, Choupo Moting/ Ramadhan Sobhi dk 61, Joe Allen, Steve Ireland na Peter Crouch/ Brian Diof dk 70

Sambaza....