Sambaza....

Mechi Bora sana kuanzia mbinu mpaka uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wametupa mechi Bora sana yenye hadhi ya UEFA Champions League

4-4-2 ya Real Madrid kama kawaida yao ni kufanya Build-up kuanzia chini kupitia kwa Viungo wao wawili(Kroos & Camavinga) na kucheza pembeni zaidi kupitia kwa Runners wao(Vinicius JR, Rodrygo + Valverde ambaye alikuwa kama Free role player)!. Hapa walifanikiwa kwenye maeneo mawili…

  1. Kuwanyima Man City uhuru wa kukimbia kwenye nafasi pembeni zaidi hasa First Half(Foden & Bernardo wakarudi kucheza karibu sana walipo Kovacic na Rodri + Stones)
  2. Kuziba haraka kwa usahihi spaces ambazo Kovacic, Rodri na Stones walihitaji kupiga pasi nyuma ya Kroos na Camavinga

Man City kwenye -3-2-4-1 in Build-up hawakuwa Bora sana kipindi cha kwanza ambacho walipiga pasi nyingi ila mpinzani wao akatumia nafasi kuchukua Mchezo

Second Half Man City walirudi tofauti hasa kuja kujibu maswali ya Real Madrid

  1. Wafanye nini kupata nafasi pembeni?

[A]: Foden, Grealish na Bernardo lazima wakimbie kwenye nafasi kwa haraka pale tu Madrid ikipoteza mpira kwenye phase ya mwisho

[B]: Kovacic, Rodri / Stones wasipige Vertical Passes nyingi sababu muda mwingi wapo Outnumbered eneo la kiungo na badala yake wapige pembeni zaidi

  1. Hawapati nafasi kuingia kwenye 18 ya mpinzani wao + kupoteza Aerial Balls nyingi kupitia Haaland, Je wafanye nini kufika kwa Lunin?

[A]: Kupiga mbali zaidi ili kupata nafasi karibu na 18 sababu Real Madrid waliacha nafasi ya Man City kupiga

[B]: Kutanua uwanja ili kupita kwenye Half Spaces na Man City ipate njia eneo la katikati hakafu wapige sana kutoka mbali

Matumizi ya nafasi na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ukaamua Mchezo kuwa na magoli mengi sana Leo (Faida kubwa ni kuwa na wachezaji wengi ambao wanapiga mbali na kukimbia kwenye nafasi)

  • Foden + Bernardo πŸ”₯ usiwape nafasi ya kupiga mbele ya 18 yako πŸ™Œ
  • Haaland Vs Rudiger πŸ”₯! Jasko Gvardiol what a player πŸ‘Š! Federico Valverde πŸ™Œ! Grealish πŸ‘πŸ‘
  • Vinicius JR 🧠 his Energy, Dribbling + Commitment πŸ”₯
  • RODRYGO GOES DA SILVA πŸ”₯ TOP TOP Talent πŸ™Œ

NB: Etihad ngoma inaanza upya πŸ˜€

FT:Real Madrid 3-3 Man City, Let’s Go

Real MadridStatMan City
14Shots12
5Shots on target6
0.63Expected goals0.86
38%Possession62%
423Passes690
11Fouls9
4Corners2
2Yellow cards2
0Red cards0

Wapwa:Anaandika @officialevodiusoscar_


Sambaza....