Mashabiki wa Wananchi Yanga
Stori

Wananchi Hii Imeenda

Sambaza....

Hatimae ile siku iliyokua inasubiriwa kwa hamu na wapenzi, wanachama na mashabiki wa Yanga ya kilele cha wiki ya Wananchi imefika. Leo July 22 Jumamosi klabu ya Yanga itahitimisha wiki ya Wananchi katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Wananchi leo watalazimikia kumiminika katika uwanja huo ili kuadhimisha siku ya Mwananchi huku wakiwa na nafasi ya kuwaona wachezaji wao wapya watakaotambulishwa sambamba na burudani mbalimbali lakini kubwa zaidi ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Yanga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Tayari klabu ya Yanga imeshatambulisha wachezaji wao wapya pamoja na jezi mpya lakini hii bado haiondoi shauku kwa mashabiki wa Yanga kujazana uwanjani na kushuhudia utambulisho rasmi wa wachezaji wao wapya kabla ya msimu kuanza.

Mahlatsi Makudubela.

Yanga tayari imewatambulisha baadhi ya nyota wake wapya kama Jonas Mkude na Nickson Kibabage lakini hamu kubwa kwa Wananchi ni kumuona winga wao mpya kutoka Afrika Kusini Mahlatsi Makudubela maarufu kama Skudu.

Tayari kocha mpya wa Yanga Miguel Gamondi jana akiongea na Waandishi wa habari alisema Kazier Chiefs ni kipimo sahihi kwao na hivyo hii imeongeza hamu ya mashabiki wa Yanga kwenda kushuhudia mchezo huo.

Sambaza....