Ibrahim Bacca akimdhibiti mshambuliaji wa Kaizer Chiefs
Stori

Yanga Yavunja Kabati, Yaweka Rekodi kwa Mkapa,

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja bila mbele ya Kaizer Chiefs katika kilele cha siku ya Wananchi na kufuta uteja wa kupoteza mechi katika siku yake.

Katika mchezo bao la Kenedy Musonda aliyeunganisha kwa ufundi mkubwa pasi ya Max Nzengeli katika dakika ya 45  lilitosha kuipa ushindi Wananchi na hivyo kumaliza sherehe zao na furaha.

Awali miaka miwili iliyopita Yanga imekua ikipata maumivu katika siku ya Wananchi, mwaka jana walifungwa na Vipers ya Uganda waka mwaka juzi walifungwa za Zanaco ya Zambia.

Katika mchezo ni kama Yanga waliamua kuonyesha vifaa vyao vyote kwani walibadili kikosi katika kila kipindi. Kipindi cha kwanza walianza kina Metacha, Kibwana, Kibabage, Job, Mwamnyeto wakati eneo la kiungo lilikua na Jonas Mkude, Mudathir, Max na mawinga Makudubela pamoja na Nkane wakati mshambuliaji akiwa ni Musonda.

Kipindi cha pili wakaingia timu nzima wachezaji 11 wengine ambapo Diara alichukua nafasi ya Metacha, wakati walinzi walikua ni Yao, Lomalisa, Fred na Bacca, viungo ni Sure Boy, Zawadi, Moloko, Farid na Ngushi huku mshambuliaji akiwa ni Mzize.

Pia walitoka Sure boy na Mzize na nafasi zao zilichukuliwa na Aucho pamoja na Aziz Ki hivyo kufanya wachezaji wote kucheza.

Sambaza....