Stori

Uongozi Simba: Njooni Simba Day Tutamtambulisha Mchezaji Wao.

Sambaza....

Klabu ya Simba leo rasmi ikiwa maeneo ya Buza imezindua wiki ya Simba kuelekea kilele cha Simba day mwaka huu ambayo itafanyika Augusti sita.

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na mashabiki wengi wa Simba, viongozi wa matawi pamoja na viongozi wa klabu msemaji wa timu hiyo alisema “Kuna mchezaji kila dirisha la usajili likifunguliwa wanamsajili lakini msimu ukianza anachezea Simba, njoo Jumapili kwa Mkapa mje mumwone,” alisema Ahmed Ally na kuongeza,

“Tumekuwa na utaratibu wa kupita eneo kwa eneo ili kuwafikia Wanasimba, kuwe kuna mabonde, milima ilimradi Wanasimba wenzetu wapo sisi tutafika ndio maana leo tupo hapa Buza. Lengo letu ni kuhakikisha tunawaalika Wanasimba mjitokeze kwa wingi kwa Mkapa siku ya Jumapili.”

Aidha pia mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtazar Mangungu ameizungumzia Simba day ya mwaka huu huku pia akijinasibu kuwa wao ndio waanzilishi wa Tamasha hilo.


“Tumeandika barua kuiomba serikali itupatie na Uwanja wa Uhuru kwa kuwa tunaamini tutaujaza Uwanja wa Mkapa mapema tu.
Tukio hili la Simba Day wengine wameiga ingawa hawataki kukiri hilo. Wameondoa neno Day wameweka Wiki,” alimalizia Mangungu.

Sambaza....