Pilato wa mechi ya Uganda na Taifa Stars awekwa wazi.
Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limewateua waamuzi kutoka nchini Gabon kuamua pambano la kundi L la kufuzu kwa michuano ya Mataifa Afrika mwakani kati ya Uganda 'The Cranes' na Tanzania 'Taifa Stars'. Mwamuzi wa kati katika pambano hilo atakuwa, Eric Arnaud Otogo Castane ambaye atasaidiwa na Mwamuzi Moussounda Montel...