Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limewateua waamuzi kutoka nchini Gabon kuamua pambano la kundi L la kufuzu kwa michuano ya Mataifa Afrika mwakani kati ya Uganda ‘The Cranes’ na Tanzania ‘Taifa Stars’.
Mwamuzi wa kati katika pambano hilo atakuwa, Eric Arnaud Otogo Castane ambaye atasaidiwa na Mwamuzi Moussounda Montel na Issa Yaya wote kutoka nchini Gabon.
Ikumbukwe Uganda watacheza na Tanzania katika uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala siku ya Jumamosi ya Septemba 8 mwaka huu.
Uganda wanashuka katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Cape Verde huku Tanzania wao wakilazimishwa sare ya bao 1-1 na Lesotho Nyumbani jijini Dar es Salaam.