Kombe la Dunia

Burundi wagundua mbinu ya Taifa Stars

Sambaza....

Nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi, Bigirimana, amewahakikishia kwa uhakika zaidi mashabiki wa nchi hiyo kuwa mechi ya Leo dhidi y Tanzania watashinda.  Akiongea na vyombo vya habari jana wakati wa mazoezi ya mwisho ya timu hiyo, amedai wao wamejiandaa kucheza mpira na kuachana na maneo maneno.

”Fyeka Burundi?!… haya ni maneno tu. Tusubirie kazi ya kesho (leo) ndani ya uwanja” Gael  Bigirimana aliwaambia waandishi wa habari huku akiilaumu kauli hiyo.

Hii ni kauli mbiu inayotumika na wadau wa mpira nchini katika kuhamasisha ushindi kwa timu ya Taifa,  ‘Fyeka Burundi’ mahususi kwaajili ya Burundi kwa sasa.

Kwa upande wa Taifa Stars, wao wapo tayari nnje na ndani ya uwanja pia. Tayari kabisa kwa mchezo wa leo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.