Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” kinakabiliwa na michezo miwili ya kufuzu kombe la Dunia kwa mwaka 2026 ambapo kitakua na michezo miwili kati ya November 18 na Novemba 21.
Kuelekea michezo hiyo dhidi ya Niger na Morocco kocha mkuu wa Taifa Stars Adel Amrouche ametaja kikosi kitakachoingia kambini hivi karibuni huku akimrudisha mlinda mlango wa Simba Aishi Manula na kiungo wa Azam Feisal Salum.