Ligi Kuu

Coastal Union waendeleza balaa Uhuru!

Sambaza....

Wagosi wa Kaya kutoka Tanga Coastal Union wameonyesha wana jambo lao msimu huu katika Ligi Kuu Bara baada ya kuendelea kupata ushindi katika michezo yake ya hivi karibuni.

Coastal Union wamejizolea alama tatu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja mbele ya “Wanalambalamba” Azam fc katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Kiungo Issa Abushehe akimkimbiza mlinzi Nicholaus Wadada wa Azam fc

Mabao ya Coastal Union yalipatikana katika kila kipindi cha mchezo huo, alikua ni Ayoub Lyanga katika kipindi cha kwanza aliewapa uongozi Coastal kabla ya Mudathir Hamis kufunga bao kipindi cha pili.

Goli la Azam fc lilifungwa na Obrey Chirwa dakika za jionii kabisa za mchezo huo. Kwa matokeo hayo maana yake kwa msimu huu Coastal wamechukua alama zote sita kwa Azam fc baada ya raundi ya kwanza kuwafunga Azam moja bila katika dimba la Mkwakwani Tanga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.