ASFC

Yanga Yakamilisha Makombe Matatu, Yatwaa FA Tanga.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kutwaa na kutetea taji lao la kombe la FA baada ya kuifunga Azam Fc kwa bao moja bila katika uwanja wa Mkakwani.

Bao la Kenedy Musonda katika dakika ya 12 akiunganisha krosi ya Djuma Shaban ndio liliamua mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wengi wa soka waliojitokeza katika uwanja wa Mkwakwani.

Baada yakutwaa kombe hilo sasa Yanga kwa msimu huu imefanikiwa kutwaa mataji mataji matatu (Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya NBC na kombe la FA) huku wakilikosa kombe la Mapinduzi na Kombe la Shirikisho Afrika walilomaliza katika nafasi ya pili.

Mshambuliaji wa Azam Fc Idris Ilunga Mbombo akimuacha mlinzi wa Yanga Ibrahim Bacca.

Vikosi vilivyokua katika mchezo wa leo

Kikosi cha Azam Fc kinachoanza! 

1. Idrissa Abdoulae
2. Lusajo Mwaikenda
3. Bruce Kangwa
4. Abdalla Kheri
5. Daniel Amoah
6. Issa Ndalla
7. Abdul Sopu
8. Sospeter Banyana
10. James Akamiko
11. Lyanga Ayoub

Sub: Masoud, Manyama, Idd Nado, Msindo, Chilambo, Dube, Mkandala, Tepsi na Kipre Jnr.

Mfumo 4:2:3:1

Kikosi cha Yanga kinachoanza!

1. Djigui Diarra
2. Djuma Shaban
3. Joyce Lomalisa
4. Ibrahim Bacca
5. Bakari Mwamnyeto
6. Dickson Job
7. Sure Boy
8. Khalid Aucho
9. Kenedy Musonda
10. Benard Morrison
11. Tuisila Kisinda

Sub: Metacha, Kibwana, Bryson, Doumbia, Mauya, Nkane, Mudathir, Bangala, Mzize

Mfumo 3:5:2

Kenedy Musonda mfungaji wa bao pekee katika mchezo wa leo.

Matukio muhimu katika mchezo huo!

1′ Mpira umeanza hapa katika Dimba la Mkwakwani Tanga.

12′ Gooaaaaaal Kenedy Musonda anaipa uongozi Yanga hapaa Mkwakwani.

39′ Kadi ya njano kwa Dickson Job baada ya kumchezea madhambi mshambuliaji Ilunga Mbombo

45+3 Mpira ni mapumziko, Yanga wanakwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja kwa sifuri.

45′ mpira umeanza tena kwa kipindi cha pili Mkwakwani.

Kiungo wa Azam Fc Sospeter Banyana akipiga mpira mbele ya Khalid Aucho

45′ Prince Dube anaingia kuchukua nafasi ya Issa Ndalla

60′ Kipre Jnr anaingia kuchukua nafasi ya Ayoub Lyanga na Bruce Kangwa anatoka kumpisha Pascal Msindo

77′ Mabadiliko Benard Morrison na Salum Aboubacar wanatoka na nafasi zao zinachukuliwa na Yanick Bangala na Clement Mzinze.

86′ Kenedy Musonda anapata kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi James Akamiko

90′ zimekamilika na mwamuzi anaongeza dakika 9 hapa Mkwakwani.

Benard Morrison akimiliki mpira mbele ya Issa Ndalla wa Azam Fc.

90+2 Anatoka Djuma Shaban anaingia Kibwana Shomary, anatoka Sospeter Banyana anaingia Idd Nado 

90+8 mpira umemalizika hapa Mkwakwani

Sambaza....