Ibrahim Bacca
Stori

Ibrahim Bacca Alivyosimika Nafasi Yake Yanga.

Sambaza....

Unapopata nafasi tafadhali fanya kama hutafanya tena. usivyoweza kufanya tena! Ibrahim Bacca kutoka Zanzibar visiwani mpaka Tanzania Bara amekuja na amebeba eneo lake peke yake.

Mohamed Nabi aliona uwezo wake akaona isiwe mbaya kumuongeza ndani ya kikosi chake na tangia hapo imekuwa muendelezo mzuri sana pale ambapo amepewa nafasi kuanzia msimu uliomalizika 2022-23.

 

Ibrahim Bacca kuanzia mashindano ya ndani mpaka ya nje huku kote anacheza kwa kiwango cha daraja la juu sana! Kachagua kuweka utofauti na kawafumba macho viongozi wa Young Africans kuhusu usajili wa beki wa kati kutoka nje ya nchi.

Nondo na JOB!. Wametengeneza ugumu na ukuta imara mbele ya Djigui Diarra lakini ongezeko la Ibrahim Bacca likapigilia muhuri wa mwisho kabisa katika eneo hilo la ulinzi. Sasa tunamuona Ibrahim Bacca mbele ya Young Africans bora kama ilivyo timu bora kwenye miguu yake.

Umri bado mdogo, nguvu na ufanisi wake ni mkubwa uwanjani huoni hata kama kuna haja ya kwenda nje na kuchukua mchezaji wa Kimataifa kwenye eneo analocheza yeye sababu anatoa ubora ambao hata wachezaji wengi wa nje hawatoi.

Ibrahim Bacca akimdhibiti mshambuliaji wa Kaizer Chiefs.

Miguel Angel Gamondi ameingia ndani ya timu lakini bado Ibrahim Bacca anatumika sababu ubora wake umeonekana na muendelezo wake ni wa kiwango cha juu katika eneo lake.

Msimu ulioisha alicheza mechi kubwa za Kimataifa na ndani ambapo uwepo wake ulipeleka uhai mkubwa sana kwenye eneo la ulinzi la Young Africans ambapo dalili zinaonekana tena kwa msimu huu atakuwa na dakika bora sana uwanjani.

Ibrahim Bacca kama hatopata majeraha yoyote kwa msimu huu naona akitoa kitu bora sana katika eneo la ulinzi kama ilivyokuwa kwa msimu uliopita.

Sambaza....