Patrice Ngoma
Tetesi

Kiungo Congo Aikataa Timu Afrika Kusini Ili Atue Yanga

Sambaza....

Kiungo wa kati Fabrice Ngoma amekataa ofa kutoka klabu ya Sekhukhune ya Afrika Kusini baada ya kuachana na Al Hilal Omdurman ya Sudan na kupelekea kuongeza nafasi ya yeye kutua Yanga.

Sekhukhune United ilifanya jaribio la kutaka kumsajili Fabrice Ngoma anayelengwa pia na Kaizer Chiefs. Kiungo huyo mrefu wa ulinzi ni mtu anayetakiwa pia na Yanga. 

Mchezaji huyo wa kimataifa wa DR Congo kwa sasa ni mchezaji huru, baada ya hivi karibuni kuachana na Al Hilal Omdurman huku akikatisha mkataba wake wa miaka mitatu na klabu hiyo kutokana na machafuko ya kisiasa nchini Sudan.

Kiungo wa Al Hilal Fabrice Ngoma (katikati) akimiliki mpira mbele ya timu pinzani

Kuondoka kwa Ngoma kutoka kwa mabingwa mara 29 wa Ligi Kuu ya Sudan kumeibua shauku kubwa kutoka kwa vilabu vya soka katika bara la Afrika kwa kuwa ni kiungo mkabaji wa hali ya juu.

Moja ya vilabu vinavyovutiwa na Ngoma ni Sekhukhune, kulingana na chanzo kisicho na shaka ambacho pia kilifichua kuwa Chiefs bado hawajaamua upya nia yao ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.

“Ndiyo, kumekuwa na nia kutoka Afrika Kusini. Sekhukhune United ilitoa ofa kwa Fabrice ambayo haikuwa nzuri vya kutosha,” chanzo kiliiambia Goal.com “Chiefs bado hawajaanza tena kutaka kumsajili Ngoma, kuna klabu za Morocco zinatarajia kumsajili na pia yupo kwenye mazungumzo na klabu za Tanzania ikiwemo Young Africans.

“Hivi karibuni atafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake,” kilimalizia chanzo hicho.

 

Sambaza....