Uhamisho

Mayele na Percy Tau Watajwa Mamelodi Sundowns

Sambaza....

Klabu ya Mamelodi Sundowns ilikosea tena taji la Ligi ya mabingwa Afrika licha ya kufanya vyema katika michuano ya Ligi ya ndani ya Afrika Kusini.

The Brazilians walitolewa nusu fainali na Wydad Casablanca kwa sare ya kusikitisha wakiwa katika uwanja wa nyumbani katika mchezo wa pili. Walipata suluhu ugenini na wakaja kupata sare ya 2-2 nyumbani.

Tovuti ya Goal.com inakuletea wachezaji ambao endapo kocha Rhulani Mokwena akiwasajili basi watwaa tena taji hilo ambalo wamelikosa kwa zaidi ya miaka mitano.

Fasika Idumba.

Sundowns mara nyingi wamekua na shida katika mipira ya juu msimu wa hivi karibuni na walihitaji beki wa kati wa ubora wa juu kama Fasika.

Uwepo wa nyota huyo wa Cape Town City uwanjani kutawafanya kuwaongezea nguzo muhimu katika kujilinda na mipira hiyo na ni jambo la kuvutia huku kumpata nyota wa kimataifa ambaye amecheza zaidi ya mechi 10 akiwa na DR Congo.

Fasika ameanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya na wachezaji wenzake wa City baada ya kukosa msimu wa 2022-23 kutokana na jeraha la muda mrefu na inasemekana kuwa mchezaji huyo mahiri anaishabikia Sundowns pia alihusishwa na Brazilians mwaka jana.

Percy Tau.

Percy Tau bila shaka, mchezaji bora zaidi katika kampeni ya Ligi ya Mabingwa 2022-23, Tau alichangia pakubwa katika kuisaidia klabu ya Misri, Al Ahly kufika fainali na kutwaa kombe hilo.

Akiwa katika kikosi cha Sundowns kilichoshinda taji la Ligi ya Mabingwa 2016, nyota huyo wa Bafana Bafana hahitaji kutambulishwa kwa kuwa amechangia mabao mengi katika msimu huu wa hivi majuzi wa Ligi ya Mabingwa akiwa na mabao matano na asisti tano.

Kumpata mchezaji kama Tau kungeongeza kwa kiasi kikubwa nafasi ya Brazilians kushinda michuano mikubwa ya kandanda kwa vilabu barani Afrika tena. Masandawana walihusishwa na Tau wakati wa usajili wa Januari 2023 na hakuna shaka kuwa Brazilians inayomilikiwa na bilionea ina fedha za kumnunua fowadi huyo wa daraja la juu kutoka Al Ahly baada ya kuripotiwa kutumia kitita cha dola milioni 3. walipomnunua.

Fiston Kalala Mayelle.

Fiston Mayele Baada ya kuooteza fomu ya kufunga kwa Cassius Mailula ambaye hana uzoefu hadi mwisho wa msimu wa hivi majuzi – Masandawana walimtegemea sana Peter Shalulile na wanahitaji mshambuliaji mwingine aliyekamilika kama Fiston Mayele.

Mayele alionyesha bila shaka kuwa yeye ni mfungaji wa mabao wa kutegemewa wa Young Africans hasa katika mashindano ya vilabu vya Afrika bara, akifunga mabao 14 ya kuvutia katika Ligi ya Mabingwa ya Caf na Kombe la Shirikisho katika msimu wa hivi majuzi na akashinda tuzo ya Kiatu cha Dhahabu.

Rais wa Young Africans, Hersi Ally Said, amethibitisha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atapatikana ikiwa ofa sahihi itatolewa na Masandawana wanapaswa kufikiria kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa DR Congo ambaye aliiwezesha Yanga kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Sambaza....