Tetesi

Nyota wa Yanga Kutimkia Ulaya

Sambaza....

Hii ni #StoriTekeTeke ambayo tumeipata, endelea kufuatilia mtandao wetu!

Mshambulizi wa kati anayechipukia wa Yanga Africans yuko katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya FC West Armenia nchini Armenia msimu ujao.

Mshambuliaji huyo mwenye kasi ataungana na FC West Armenia ambayo hivi majuzi ilipandishwa kwenye ligi kuu ya nchini Armenia.

Yusuph Athuman, aliyejiunga na Yanga akitokea Biashara United anakwenda kuimarisha safu yao ya ushambuliaji ya timu hiyo akiungana na Erick Mwijage wa Kagera Sugar katika timu hiyo ambae pia amesajili wa na timu hiyo ya Ulaya Mashariki.

Yacouba Sogne na Yusuph Athuman.

Akizungumzia uhamisho huo nyota huyo aliiambia FAR Post “Kwanza Mwenyezi Mungu ni juu ya kila kitu. Ni ndoto ya kila mchezaji wa Kiafrika kucheza Ulaya,” alisema na kuongeza

“Ni nafasi nzuri sana kwangu na ni hatua nzuri kuelekea malengo yangu. Namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi hii ya kwenda kuonyesha kipaji changu katika soko la thamani zaidi duniani,” alisema

Sambaza....