Baadhi ya viongozi wa Yanga
Tetesi

Rasmi Yanga Wamkosa Straika wa Mabao.

Sambaza....

Marumo Gallants wamethibitisha kuondoka kwa Ranga Chivaviro kwenda kwa wababe wa Soweto Kaizer Chiefs. Chivaviro alikuwa mshambuliaji muhimu kwa Gallants msimu uliopita Mkataba wake ulimalizika Juni 30.

Chivaviro alikuwa amehusishwa na timu kadhaa baada ya kiwango chake cha juu akiwa na Gallants msimu uliomalizika wa 2022/23. Miongoni mwao walikuwa vigogo wa Tanzania Yanga SC na Vigogo wa Soweto Orlando Pirates.

Hata hivyo, Chiefs wameshinda mbio za kumnasa mshambuliaji huyo ambaye anatajwa kuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika na timu hiyo ya zamani ya Ligi Kuu ya Soka ya Afrika Kusini.

Rango Chivaviro

Gallants wamethibitisha wachezaji walioachana na timu hiyo, miongoni mwao ni mwenye umri wa miaka 30 ambaye anatajwa kutambulishwa na Glamour Boys.

Kuwasili kwa Chivaviro kunaweza kuwa mwisho wa Caleb-Bonfils Bimenyimana huko Amakhosi. Raia huyo wa Burundi alitatizika kupata fomu nzuri katika klabu hiyo na ripoti zinasema yuko njiani kuondoka.

Chivaviro alifunga mabao 10 katika mechi 19 za PSL msimu uliopita na saba katika mashindano 10 ya Kombe la Shirikisho la Caf. Washabiki wakongwe wa Amakhosi wanatumai kuwa mshambuliaji wao mpya anaweza kuwasaidia kunyakua fedha katika msimu wa 2023/24.

Chanzo: Goal.com

Sambaza....