Saidoo Ntibazinkiza na Pape Osmane Sakho
ASFC

Simba kushuka dimbani katika uwanja mpya

Sambaza....

Raundi ya nne ya kombe la Azamsports Federation Cup inaendelea wiki hii na inaanza kesho ambapo Simba watashuka dimbani kuendeleza walipoishia.

Wekundu wa Msimbazi Simba watawakaribisha Afrikan Sports “Wanakimanumanu” kutoka Tanga katika uwanja wa Uhuru na si Benjamin Mkapa kama ilivyo kawaida kwa Simba kucheza katika uwanja huo kama uwanja wao wa nyumbani. 

Mchezo huo utakaopigwa saa kumi jioni kama Simba itafanikiwa kuibuka na ushindi watakata tiketi yakwenda robo fainali ya michuano hiyo ambayo msimu uliopita waliishia hatua ya nusu fainali kwa kutolewa na Yanga.

Simba baada yakulikosa kombe hilo mwaka jana ambao waliingia kama mabingwa watetezi ni wazi hawatakua tayari kulikosa tena msimu huu kwani ndio kombe pekee ambalo wana matuamini yakulichukua msimu huu. Kwenye ligi tayari wana nafasi finyu yakutwaa ubingwa na tayari wameshaachwa alama nane na watani zao Yanga wanaoongoza Ligi.

Sambaza....