Stori

Yanga na Jack Wilshere wao!

Sambaza....

Unamkumbuka kiungo fundi wa Kiiengereza Jack Wilshere!? Kipaji maridhawa kutoka katika ardhi ya Malkia lakini kikapotelea katika majeruhi.

Moja ya kazi nzuri ya kuibua vipaji kutoka babu Wenger lakini juzi tu alitangaza kuachana na soka na kuhamia kwenye umeneja na timu yake ya zamani Arsenal ikampatia kazi katika timu za vijana.

Jack Wilshere.

Nasikitika sana kuona dogo anaondoka Yanga japo najua hakuna mchezaji wenye kudumu maisha yake yote katika soka au timu.

Kuna muda utaachana na timu au muda wako utakuwa umepita zamu ya wenzako na sababu nyingi huwa zipo za mchezaji kuachwa na klabu yake. Kama vile kuporomoka kiwango, nidhamu na majeraha ya mara kwa mara kumalizika mkataba na tathimini kuonesha huna kipya anachoweza kukitoa.

Balama Mapinduzi.

Lakini si kwa bwana mdogo huyu ambaye aliumia mara moja (hana historia ya kuwa majeruhi) zaidi ya hiyo mara moja iliyotaka kutishia soka lake japo klabu ilimvumilia sana sana maana yake wamemtathimini kwenye kiwango chake kushuka.

Nirejee kwenye kile kitu nilichotaka kukisema, nakumbuka niliandika uchambuzi wangu kuhusiana na wachezaji wageni waliojiunga Yanga dirisha dogo ambao walipata nafasi ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni, kama Ibrahim Bacca, Chico Ushindi, Sure Boy na Mapinduzi Balama mwenyeji ambaye alikuwa anarudi kama mgeni baada ya muda mrefu.

Balama Mapinduzi.

Nilianza kuiona safari ya Balama kuwa ngumu ya kuendelea kubaki Yanga nilikuwa na hoja za kiufundi lakini ‘Wanazuoni ‘ walikuja juu na kuponda uchambuzi wangu huku wakiita wa ‘mchongo’.

Nasikitika kama kaka mtu kuona dogo anaondoka kwenye klabu kubwa ambayo ingemsogeza hatua kadhaa za kimaisha ikifananisha na timu nyingine.

Adui namba moja wa wachezaji ni majeruhi. Majeruhi yanaweza kumaliza “Career” yako hata kama umri bado. Balama ana nafasi ya kupiga U-turn kwa kupitia timu nyingine akaja tena kwenye timu kubwa na kwa bei mbaya kwa sababu ni kipaji halisi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.