ASFC

Yanga Wanasaka Rekodi, Geita Wanaingia na Kisasi

Sambaza....

Mchezo wa mwisho wa robo fainali ya FA utapigwa leo baada ya michezo mingine mitatu kumalizika na kupata timu tatu zitakazocheza nusu fainali sasa leo ni zamu ya Wananchi Yanga dhidi ya wachimba dhahabu Geita Gold.

Yanga watawakaribisha Geita Gold leo saa mbili usiku katika Dimba la Azam Complex Chamanzi katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali na wakusisimua kutokana na jinsi ambavyo timu zote mbili zimejiandaa na mchezo huo.

 

Tayari Simba, Azam na Singida Big Stars zimeshafuzu kwa hatua ya nusu fainali na mshindi wa mchezo huo kati ya Yanga na Geita ndio atakwenda kukutana na Singida katika nusu fainali.

Yanga mabingwa watetezi wa kombe hilo wataingia dimbani wakisaka kuendeleza rekodi yao nzuri katika michuano hiyo ambapo mpaka sasa wamecheza nusu fainali mara tatu mfulilizo na hivyo wakifuzu na leo itakua ni mara ya nne mfululizo.

Yanga itaingia dimbani leo ikiwa na jeshi lake kamili kwani hata Benard Morisson amepona majeraha yake hiyo yupo tayari kutumika katika mchezo wa leo, mchezaji pekee mwenye wasiwasi wa kukosekana leo ni Fiston Mayele ambae huenda akapumzishwa kutokana na uchovu akiandaliwa kuwauwa Simba April 16.

Kwa upande wa Geita wao bado wanakumbuka walivyofungwa nje ndani na Yanga msimu huu lakini pia walovyotolewa msimu uliopita katika michuano hii hii hatua ya robo fainali na Wananchi Yanga.

Hivyo Geita leo wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu mbaya yakupoteza mbele ya Yanga lakini pia wakitaka kuandika historia mpya mbele ya wababe hao wa Jangwani. Ushindi katika mchezo huo kwa Geita una maana kwamba watakua wamfuzu kucheza nusu fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Sambaza....