Ligi Kuu

Mambo matano niliyojifunza katika mchezo wa Simba na Yanga!

Sambaza....

1: Tuna safari ndefu sana kuifikia pepo kama bado tunaamini giza lina nafasi kubwa katika mpira wetu. Ni ngumu kujenga timu yenye ushindani kimataifa kwa kuamini katika nguvu za giza kama ndiyo njia sahihi kwetu sisi kutupa ushindi.


2: Inawezekana Beno Kakolanya kaimbwa sana kuliko mchezaji yeyote katika mechi ya Jana. Hapana shaka alistahili kuwa nyimbo pendwa kwa sababu ya kiwango chake alichokionesha jana. Ndiye alikuwa muhimili mkubwa jana, kila washambuliaji wa Simba walipokuwa wanawapita kina Yondani walipokuwa wanakutana na Beno Kakolanya walikuwa wanakutana na mabeki wawili wa kiwango cha Puyol , Ramos pamoja na kipa mmoja.


3: Inawezekana kipindi cha Kwanza Simba walitawala sana eneo la katikati kwa sababu walikuwa na aina ya wachezaji ambao wanauwezo mkubwa wa kumiliki mpira (Jonas Mkude, Chama na James Kotei) lakini Yanga walitumia silaha ambayo iliwalinda sana mwanzo hadi mwisho wa mchezo , nayo ni kumtumia Ninja kama beki wa ziada aliyecheza katika eneo la kiungo wa kuzuia.


4: Emmanuel Okwi alikuwepo, Meddie Kagere pia alikuwepo. Uwepo wao ndani ulizidi kuonesha umuhimu wa John Bocco. Kiongozi, na mpambanaji mkubwa katika eneo la mbele. Alikosekana huyu, Emmanuel Okwi aliijaribu hii kazi lakini kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda kasi yake ilikuwa inapungua sana.


5: Natamani baada ya mechi ya jana Faisal angemfuata Mkude aongee naye vizuri. Amuulize maswali mengi kuhusu eneo ambalo alikuwa anacheza kwa kifupi maswali yake angeyajumuisha kwa pamoja na kuyaweka kwenye swali moja , Kaka kwanini wewe ni kiungo bora wa kati wa kizazi hiki ?

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x