Fiston Mayele akishangilia bao lake dhidi ya Singida Big Stars
Tetesi

Adebayor Kutua Simba, Mayele Hakijaeleweka Bado.

Sambaza....

Tovuti yako pendwa ya Kandanda.co.tz inakuletea vichwa vya habari vilivyogonga katika magazeti na mitandao mbalimbali.

Simba Sc imekubaliana na mshambuliaji wa RS Berkane mkataba wa miaka miwili na hivyo sasa uongozi wa Simba unapaswa kumalizana na wenzao wa Berkane ili kumaliza usajili huo [Sport Xtra]

Ismail Aziz Kader amejiunga na JKT Tanzania timu iliyopanda daraja msimu huu. Kader ameachana na Azam Fc baada ya kumaliza mkataba wake [Mwanaspoti]

David Kameta

Azam Fc inamtaka mlinzi wa kulia David Kameta Duchu ambae alikua anaitumikia Mtibwa kwa mkopo akitokea Simba. Pia timu yake Simba imeonyesha nia yakutaka kumrudisha nyota wake huyo waliemsajili kutokea Lipuli fc. [Mwanaspoti]

Joyce Lomalisa ametaja sababu inayomuondoa Yanga akisema hafurahishwi na kukaa benchi na kumuona Kibwana Shomary akicheza ambae kiasili si mlinzi wa kushoto. Uongozi wa Yanga wao wamemwambia ailete timu mezani inayotaka huduma yake. [Sport Xtra]

Simba mpaka sasa imeachana na Victor Akpan, Augustine Okrah na Mohamed Outtara rasmi. Bado wapo kwenye mazungumzo na wachezaji Joash Onyango na Nelson Okwa ya kutafuta njia sahihi ya kuachana.

Nelson Okwa (mbele) akishangilia bao pamoja na Victor Akpna Pape Sakho

Usajili wa msimu huu rasmi utafunguliwa July mosi na kufungwa August 30 mwaka huu. Hivyo zimebaki siku kumi kuelekea kufunguliwa kwa usajili huo wa wachezaji.

Nyota wa Yanga Fiston Mayele amesema hatma yake ipo mikononi mwa timu yake huku yeye akiwa tayari ameweka wazi yupo tayari kupokea ofa nono zaidi itakayokuja ama hata kutoka kwa klabu yake Yanga.

 

 

Sambaza....