Kocha mpya wa Yanga Miguel Gamondi akiwa mazoezini na wachezaji wake
Stori

Gamondi Alivyotibu Tatizo Lililomshinda Nabi na Wenzake

Sambaza....

Miaka miwili mpaka mitatu iliyopita Young Africans ilikuwa na idadi ndogo ya watu ambao wanaipa timu mabao mengi kwa msimu mzima wa mashindano lakini sasahivi imekuwa tofauti.

Tuanzie msimu wa 2018-19 Heritier Makambo alifunga mabao 21 na pasi za mabao 4 ndani ya mechi 39 za mashindano yote kabla ya kwenda Horoya AC na baadae walipokuja kina Yikpe, Molinga, Balinya, Sibomana na wengine bado ikawa shida kuipa timu namba nzuri kwenye ufungaji.

 

Wakati huo ni msimu ambao Simba SC walikuwa na namba nzuri kwenye ufungaji, kuanzia eneo la nyuma mpaka mbele walikuwa na idadi nzuri ya watu ambao wanafunga mechi baada ya mechi kama Emmanuel Okwi, John Bocco, Meddie Kagere, Clatous Chama, Luis Miquissone na wengine.

Ndani ya hiyo miaka Simba walikuwa na wachezaji watatu mpaka wanne ambao walikuwa na uwezo wa kufunga zaidi ya mabao 10 ndani ya msimu mmoja kitu kilichofanya kuwa klabu inayofunga magoli mengi ndani ya Ligi Kuu ya Tanzania.

Leo hii pale Young Africans naona kuna faida kubwa ambayo anaipata Miguel Gamondi ndani ya kikosi chake kwa kuangalia ubora wa timu kwenye ufungaji mpaka hivi sasa, kuna mtawanyo wa magoli kwa wachezaji wengi kwenye maeneo tofauti ndani ya uwanja.

Clement Mzinze akishangilia bao na wachezaji wenzake katika mchezo dhidi ya El-Merreck.

Miaka miwili iliyopita timu ilikuwa inamtegemea Fiston Mayele kwenye eneo la mwisho kama mtu ambaye ndiye “Top Scorer” wa Klabu yao, lakini hivi sasa timu inatoa mwanga mzuri sababu kuna idadi ya watu wengi ambao wanafunga.

Max Nzengeli, Pacome Zouzoua, Kennedy Musonda, Aziz KI, Clement Mzize hawa wote naona miguu yao ina magoli mengi ya Young Africans msimu huu ukiunganisha na wengine ambao wana uwezo wa kuweka mpira wavuni kutoka kwenye nafasi tofauti tofauti.

Miguel Gamondi kama timu yake itaendelea kufunga hivi basi naona msimu huu watakuwa na namba nzuri kwenye ufungaji kama ilivyokuwa kwa wapinzani wao Simba SC kwa takribani misimu minne.

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x