Sambaza....

Wapwa, nionavyo mimi kile kinachoenda kutokea kwa Mayele anapoondoka Yanva ndiyo kile kilichotokea kwa Kipre Tchetche Azam wakati ule.

Sina maana nyingine yeyote zaidi ya kukumbukwa kwa miaka kadhaa mbele baada ya kuondoka kwao kwenye vilabu hivi viwili vya Tanzania.

 

Ni ukweli usiofichika Kipre hadi leo anaimbwa na mashabiki wa Azam ikiwa ni zaidi ya miaka 8 tangu kuondoka kwake mwaka 2016.

Lakini utajiuliza kwanini anatajwa sana ilhali hata wachezaji wengine wazuri wanaokuja pale lazima watu wajiulize kwamba anacheza vizuri kama Kipre!?

Kipre (katikati)

Ndiyo kitu kinachokuja kwa Mayele Kwa sasa kila mchezaji mgeni hasa wa safu ya washambuliaji atakuwa anafanyiwa mlinganisho naye kutokana na alama aliyoiacha kwa miaka miwili aliyekuwepo hapa nchini.

Hii haiji kibahati mbaya’ performance’ yake ndiyo siri ya hili jambo kama ambavyo kinyume chake ukishindwa kufanya vizuri utaacha alama yako ya washindwa.

Fiston Mayele akishangilia bao lake dhidi ya Singida Big Stars.

Mfano Kindoki ukimtaja tu, moj kwa moja unamaananisha kipa ambaye hakufanikiwa pale kwa Wananchi wakati akiwepo nchini akiwatumikia.

 

Sambaza....