Alli Kamwe msemaji wa klabu ya Yanga
Ligi Kuu

Alli Kamwe: Tunajua ni Mechi Kubwa Lakini Hatuifikirii Simba

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa Dabi ya Kariakoo Msemaji wa Klabu ya Yanga Alli Kamwe ameonekana kumjibu mwenzake wa Simba Ahmed Ally baada ya kuwahimiza wachezaji wake kuandika historia kwa kuifunga Yanga.

Ally amesema amesikia alichosema Ahmed Ally na amefurahi kusikia wenzao wakiwahimiza wachezaji wao kuandika historia kwa kuifunga Yanga. Mara ya mwisho kwa Simba kuifunga Yanga katika Ligi ilikua ni mwaka 2019 kwa bao pekee la Meddie Kagere.

 

Alli Kamwe “Moja kati ya jambo lilinipa raha leo ni kuwasikia ndugu zetu [Simba]  wakiwaambia wachezaji wao waende wakapambane waifunge Yanga ili waingie katika historia,” alisema na kuongeza

“Maana yake ndugu zetu wale faraja yao ni kuifunga Yanga, hawana jambo jingine lolote wanalolitafuta zaidi ya kumfunga Yanga. Hili jambo waliliahidi katika uchaguzi na watu wakachaguliwa lakini pia na leo wamewaambia wachezaji wao,” aliongeza.

Kamwe pia amesema kwa sasa hivi wao wanakwenda kuingia katika mchezo huo bila kuifikiria Simba kwani wana wachezaji wakubwa ambao wanajua nini wafanye hivyo mchezo huo ni kama maandalizi ya mchezo wao wa robo fainali.

“Sisi tunacheza hatuwafikirii wao sisi tunacheza kuangalia ubingwa wa Ligi, tunacheza huku tukiwa tunajiandaa na mchezo wa robo fainali ya Shirikisho Afrika. Tunajua ni mchezo mkubwa lakini ukiwa na hazina ya wachezaji wakubwa Afrika hutakiwi kuwa na presha,” alimalizia Alli Kamwe

Sambaza....