Ligi Kuu

Bocco: Mashabiki njooni uwanjani muone!

Sambaza....

Nahodha wa Timu ya Simba, John Bocco amesema wamejipanga kuhakikisha wanaondoka na alama zote sita katika michezo miwili dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons.

Bocco amesema hayo kabla ya kuondoka alfajiri leo Jumatatu Juni 22, kuelekea jijini Mbeya huku akiweka wazi kuwa wachezaji wana ari na kila mmoja anahitaji ushindi kwenye mechi hizo.

Wachezaji wa Simba wakiwa wamewasili Songwe Internationa Airport.

Nahodha amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika michezo hiyo ili kuwatia nguvu na hatimaye kwa pamoja lengo la kupatikana kwa pointi sita lifanikiwe.

“Mpaka muda huu tunaondoka wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na lengo la kila mmoja ni kupata alama zote sita katika michezo miwili.

John Raphael Bocco akiwa uwanja wa ndege.

Tunafahamu mechi zitakuwa ngumu kwa kuwa kila timu inahitaji pointi tatu katika kipindi hiki ligi ikielekea ukingoni lakini sisi tumejipanga kukabiliana na chochote kitachotokea ili kupata pointi zote,” amesema Bocco, ambae ameongea hayo alipokua akizungumza na tovuti rasmi ya klabu.

Jumatano wiki hii kikosi Simba sc itashuka  katika Uwanja wa Sokoine kuikabili Mbeya City na mwishoni mwa wiki itacheza na Prisons zote za jijini Mbeya.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.