Tetesi

Dili la Yanga na Yacoub Sogne limebuma ?

Sambaza....

Afisa habari wa Yanga , Hassan Bumbuli kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini aliripoti kuwa leo tarehe 27/08/20120 mshambuliaji Yacoub Sogne angetua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere.

Lakini kwa bahati mbaya hajufanikiwa kuja nchini. Baadaye afisa uhamasishaji wa klabu ya Yanga , Antonio Nugaz alidai kuwa hakuna taarifa yoyote rasmi iliyotolewa na Yanga kuhusu ujio wa Yacoub Sogne.

Kuna taarifa zinazidi kuenea zinadai kuwa Yanga imeshindwa kumalizana na Yacoub Sogne hivo kuna uwezekano mkubwa wa Yanga kutomsajili Yacoub Sogne.

Taarifa hizi zinazidi kuipa nafasi kubwa habari ya Jacky Tusiyesenge. Yanga wanaripotiwa kuwa katika mazungumzo ya mwisho na Jacky Tusiyenge hivo anaweza kuwa mbadala wa Yacoub Sogne


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.