Alejandro Ganarcho
Stori

Garnacho: Mali ya Argentina Iliyoikataa Hispania.

Sambaza....

Kipaji walichokipoteza Atletico Madrid Alejandro Garnacho Ferreyra (19), moja ya vijana wanaokuja vizuri sana katika soka la Ulaya.

Mzaliwa wa Hispania pale jijini Madrid na alikulia kwenye Academy ya Atletico Madrid hadi alipojiunga na Mashetani wekundu mwaka 2020 akiwa na umri wa miaka 16 tu.

Unabaki kujiuliza alifikaje Argentina? Baba yake na Garnacho ni Muhispania halisia kabisa na mama yake Garnacho amezaliwa Amerika Kusini katika nchi ya Argentina, hii ndio sababu ya yeye kuichezea Argentina.

Alejandro Ganarcho (kulia).

Uwezo wake na ufundi wake mguuni hasa pale anapokuwa na mpira utabaki ukisema hakika hii ni zawadi kwa taifa la Argentina.

Moja ya mahojiano ambayo alifanyiwa Alejandro Garnacho aliwahi kusema “Scaloni aliniuliza kama nina wasiwasi, akaniambia nitulie, nicheze ninavyojua na atanipa nafasi na huwa ninapocheza soka nijaribu kuwa mimi. Pia wachezaji wenzangu nao wananisaidia ikiwa mazoezini hata kwenye mechi za kimashindano,” 

Ni mmoja wa vijana wenye umri mdogo na wenye kiu ya mafanikio watakaokuja kusumbua baadae. Sio kwa Manchester United tu hata kwenye Taifa lake la Argentina akiwa na  wenzake kina  Alex Mac Allister, Enzo Fernandez, Julian Alvarez, Nahuel Molina, Lisandro Martinez, Federico Redondo n.k.

Alejandro Ganarcho akiitumikia Argentina.

Kwa pesa ambayo Manchester United wametumia kumsajili Garnacho unaweza sema ni kama wamemchukua bure tu. Kiasi cha €465,000, hii ni takribani 1.2B ya Kitanzania. Kwa soko la usajili Ulaya lilivyo kwa sasa ni pesa ndogo mno.

Amemfuata Mama alipo.
Siri ambayo wengi hawaijui kuhusu kijana huyu, mataifa mawili huko nyuma Hispania na Argentina yalikuwa yakimgombania kabla ya yeye kufanya maamuzi juu ya hatma yake ya Taifa gani atalitumika.

Garnacho ameliwakilisha Taifa la Hispania katika timu za chini ya miaka 18 na ameliwakilisha taifa la Argentina chini ya katika timu ya chini ya miaka 20, na sasa imekua rasmi Garnacho atalitumia taifa la Argentina baada kucheza kwenye kikosi cha wakubwa.

Alejandro Ganarcho.

Kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Australia ambapo Argentina aliondoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2 kwa 0  Alejandro Garnacho aliingia na kucheza katika mchezo huo.

Alejandro Garnacho Mali Ya Argentina 🇦🇷👋.

Abuu Mwakyoma

Sambaza....