Himid Mao akisaini katika klabu yake mpya
Uhamisho

Himid Mao Atimikia Timu Mpya Misri

Sambaza....

Kiungo wa timu ya Taifa ya Tanzania Himid Mao Mkami ameachana na klabu yake ya GhazL El-Mahalla iliyoshuka daraja aliyoitumikia msimu uliopita na kujiunga na Tala’a El Gaish.

Himid Mao ataungana pia na nyota mwenzie wa El Gaish  Ahmed El Shekhe, Himid anakweda huko baada ya  mkataba wake na Ghazl El-Mahalla kukamilika mwishoni mwa msimu wa 2022/23. Mao, mwenye umri wa miaka 30, alitumia misimu miwili iliyopita huko El-Mahalla.

Himid Mao

Himid akiwa pia amechezea vilabu vya Petrojet, ENPPI, na Entag El-Harby. Kwa ujumla, Mao, ambaye ameichezea timu ya Taifa ya Tanzania michezo 66, alicheza mechi zaidi ya 135 nchini Misri ambapo alifunga mabao sita tangu kuwasili kwake akitokea Azam FC.

Himid Mao amekua na nyakati nzuri nchini Misri ambapo licha ya vilabu ambavyo amekua akivichezea vimekua vikishuka daraja lakini yeye amekua akisajiliwa na kubaki Ligi Kuu.

Sambaza....