Stori

Kaizer Chiefs: Simba ni Kubwa Kuliko Yanga Lakini Hatuwachukulii Poa.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Kaizer Chiefs tayari imetua nchini kuelekea katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao Yanga katika kilele cha siku ya Mwananchi July 22 mwaka huu.

Chiefs ambao wamefanya usajili wa kutisha akiwepo Ranga Chivaviro ambae yupo pamoja na timu alisema “Ninajisikia vizuri kuwa hapa, nimerudi tena,” alisema na kuongeza

“Mara ya mwisho nilipokuwa hapa, kila mtu alinikaribisha vizuri sana. Ninahisi furaha kuwa Tanzania. Sitarajii chochote zaidi ya mashabiki kujaza uwanja, nafurahiya kuwa Tanzania. Nilipata msisimko [wakati mwaliko ulipokuja] kwa sababu najua watu wa hapa wanapenda soka,” alisema Chivaviro.

Ranga Chivaviro (kushoto) akichuana na Yanick Bangala katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika

Nae nahodha wa Chiefs Itumeleng Khune alisema hawatawachukulia poa Yanga na hawatalichukulia poa pambano hilo dhidi ya Yanga.

“Sio mara yetu ya kwanza kuja Tanzania, tulikuja kucheza na Simba, ambayo ni klabu kubwa, kama vile Yanga ni klabu kubwa pia,” alisema Khune. “Pia tunajiandaa kwa msimu mrefu sana. Sisi ni klabu kubwa nchini Afrika Kusini yenye mashabiki wengi. Ni wazi mashabik wanaifuata klabu popote inapokwenda. 

Yanga wanatarajia kushuka uwanjani siku ya kesho saa moja kamili usiku kuwakabili Kaizer Chiefs katika mchezo wa kirafiki ambao kwa kiasi kikubwa utatoa sura ya timu yao kuelekea michuano ya Kitaifa na Kimataifa kwa msimu ujao.

Sambaza....