Mlinzi wa Simba Henock Inonga Baka akishangilia bao la kwanza la Simba katika mchezo dhidi ya Yanga walipokutana mara ya mwisho katika Ligi
Ligi Kuu

Kocha Simba: Goli la Inonga Ulikua ni Mpango wa Timu

Sambaza....

Baada ya ushindi wa mabao mawili kwa sifuri mbele ya Watani zao Yanga kocha msaidizi wa klabu ya Simba Juma Mgunda amejinasibu kwamba yote yale yaliyotokea ulikua ni mpango wa timu nzima.

Juma Mgunda amesema walipanga kupata bao la mapema katika mchezo ule ili waweze kuwatoa Yanga mchezoni kwa haraka na kuwapelekea kupata ushindi katika mchezo huo.

“Mpango wetu ulikuwa ni kupata bao la mepema, kocha mkuu Robertinho alituambia jana kabla ya mchezo tunahitaji kufanya hivyo,” alisema Juma Mgunda.

Nyota huyo wa zamani wa Coastal Union hakuacha kuwapa sifa na kuwashukuru wachezaji wao maana ndio kwa kiasi kikubwa walipelekea timu kuibuka na alama tatu katika mchezo huo muhimu.

Henock Inonga Baka akipiga kichwa na kufunga bao la kwanza mbele ya walinzi wa Yanga

Juma Mgunda “Nichukue nafasi hii kuwapongeza wachezaji wetu kwa kufuata maelekezo waliyowapa, haikuwa mechi rahisi lakini jambo bora tumefanikiwa kushinda na kupata pointi tatu muhimu.”

Katika mchezo huo wa jana Simba walianza kwa kupata bao kupitia kwa Henock Inonga katika dakika ya pili tu ya mchezo kabla ya Kibu Denis kufunga bao la pili dakika ya 32.

Simba hatimae imefuta uteja mbele ya Yanga baada ya kushindwa kupata ushindi kwa miaka mitatu mfululizo kwenye mechi za Ligi Kuu. Mara ya mwisho Simba kumfunga Yanga ilikua ni February 2019 katika mchezo wa Ligi Kuu.

Sambaza....