ASFC

Miraj Athuman na rekodi ya kutisha!

Sambaza....

Mshambuliaji wa zamani Simba sc Miraj Athuman “Shevishenko” anatarajiwa kuandika rekodi  ya aina yake kuelekea katika mchezo wa fainali wa Azam Sports Federation Cup dhidi ya Namungo fc.

Baada ya Simba kuifunga mabao manne kwa moja Yanga na kukata tiketi ya kwenda fainali  ya kombe la FA imekua ni habati na historia kwa upande wa wachezaji Shevi na Haruna Shamte.

Miraji Athumani “Sheva”

Haruna Shamte na Miraji Athuman msimu uliopita wakiwa na Lipuli fc walifanikiwa kuingia fainali ya FA na kupoteza mbele ya Azam fc, lakini msimu huu wawili hao wanaitumikia Simba sc na tayari imeingia fainali ya kombe hilo.

Hivyo endapo Shamte na Miraj watacheza mchezo huo wa fainali watakua wamecheza fainali ya FA kwa misimu miwili mfululizo ambayo mashindi wake ataiwakilisha nchi katika michuano ya CAF Confederarion cup.

Simba sc itacheza fainali ya kombe la FA dhidi ya Namungo fc katika uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa August 02 mwaka  huu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.