Clement Mzize
Stori

Ni Mzize Sio Musonda Atakaeziba Nafasi ya Mayele

Sambaza....

Mchezo dhidi ya Azam FC kwenye Ngao ya Jamii siku ya Jumatano timu ilihitaji mtu wa kupiga kwa usahihi zaidi eneo la mwisho na aliingia akafanya hivyo.

Timu ilihitaji mtu anayeweza kugombania mpira dhidi ya wachezaji au walinzi wa timu pinzani na kufanya kitu bora zaidi mbele yao, huyu akaingia na kufanya hivyo.

 

Bado haikutosha walihitaji mchezaji anayeweza kukaa eneo gumu na akapokea mpira kisha kufanya maamuzi kwa usahihi pia alifanya hivyo dhidi ya Azam FC. Kwanini Clement Mzize?

Rahisi! Clement Mzize ni mchezaji ambaye anastahili kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Young Africans msimu huu! Fiston Mayele ameondoka Hafidh Konkoni yupo ila anahitaji muda zaidi, mchezaji wa uhakika pale ni Kennedy Musonda.

Mohamed Nabi alimtambulisha na ameondoka kamuacha ndani ya klabu kilichobaki ni makocha waliopo kuendeleza ubora wa kipaji hii pale Young Africans! Miguu yake ina kitu bora sana ndani yauwanja hata kwa dakika chache ambazo hupewa huwa anafanya kitu bora sana.

Clement Mzize na Kenedy Musonda.

Binafsi naamini kama atapewa nafasi zaidi kwenye msimu huu wa mashindano basi Young Africans itanufaika na miguu yake kwenye eneo la mwisho akiwa pembeni ya wachezaji wengine kama Kennedy Musonda na Aziz KI.

Mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC aliingia na kubadilisha taswira ya mchezo kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la mbele, hata mechi nyingi za msimu uliopita alifanya kitu bora sana ndani ya dakika alizopewa na Mohamed Nabi.

Vizuri! Young Africans ina wachezaji wageni wenye ubora katika eneo hilo lakini bado naamini kutokana na uwezo wa Clement Mzize ana nafasi kubwa tu ndani ya kikosi cha Young Africans.

 

Sambaza....