Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani Haji amesema kuwa ili uweze kupata tiketi unahitaji kuwa na N-card ambayo gharama yake ni 1,000 na gharama ya tiketi ni 5,000.
Miaka 30 imepita tangu nchi hii ikaribie kubeba kombe la Afrika, mara ya mwisho ilikua ni 1993 sasa fikiria nchi imekaa muda wote huo bila kufika fainali.
Matajiri hao wa Misri wanatumia uwanja wa 30 June wanawajua vizuri Yanga kwani tayari walishakuka nchini kucheza na Wananchi na walifanikiwa kuwaondosha Yanga katika Playoffs ya Kombe la Shirikisho