Tahariri

Iko Wapi Thamani ya Mashabiki?

Sambaza....

Kipenda roho hula nyama mbichi. Mtu anapopenda kitu kiasi kwamba akashindwa kuzificha hisia zake za upendo juu ya kitu fulani basi humgharimu muda, mali, fedha na wakati mwingine kupoteza uhai sababu ya mahaba na kitu.

Shabiki ni mtu anayependa kitu au jambo na kulifuatilia na Soka ndo mchezo pendwa zaidi ulimwenguni hivyo una mashabiki na wafuatiliaji wengi. Shabiki ana mchango mkubwa katika maendeleo ya vilabu na mchezo wenyewe.

Hivyo shabiki ni wa thamani sana kwani yeye ndio soko, shabiki hununua jezi, tiketi na huenda uwanjani kutia shime na kushangilia timu zao.

Mashabiki wa klabu ya Simba.

Lakini stori ni tofauti hapa nchini (Tanzania), licha ya kuwa na mashabiki wengi wa soka lakini hawapewi thamani, hawapewi ule ufahari na huduma msingi wanazotakiwa kupata wakiwa nje na hata ndani ya viwanja.

Mashabiki wamekua wakikumbwa na kadhia mbalimbali mfano ulinzi mdogo wawapo uwanjani, ugawaji na utaratibu mbovu wa upatikanaji tiketi, utaratibu mbovu wa kuingia viwanjani umekua na karagha kiasi cha kusababisha mashabiki kufanya vurugu ili kuingia viwanjani na suala hili limechagiza sana kupunguza idadi ya mashabiki kwenda viwanjani.

Mfano katika mchezo wa fainali ya kwanza kati ya Yanga na USM Algers licha ya mashabiki kujitokeza kwa wingi sana, iliwalazimu mashabiki kufanya fujo ili kuingia uwanjani na hii ilitokana na kuchelewa kufunguliwa mageti ya uwanja na utaratibu mbovu wa ugawaji tiketi za promotion(bure).

Mashabiki waliojitokeza katika mchezo wa leo wa Yanga dhidi ya USM Algier.

Haya yote yanasababishwa uwajibikaji hafifu wa mamlaka za soka zinazomiliki viwanja pamoja na vilabu. Juhudi ni ndogo za kuhakikisha shabiki anakua salama angiapo na atokapo viwanjani ni kama wanafanya kazi kimazoea, yaaani liwalo na liwe na kwasabu mashabiki wanazipenda timu tao basi wanakubali kadhia na fedheha sababu mamlaka zinazohusika hazioni thamani yao na hii mbaya kwa ustawi wa soka letu kwani kunamfanya shabiki asitamani kwenda uwanjani ili kukwepa kadhia hizi.

Vilabu na mamlaka za viwanja pamoja na shirikisho wakae chini waweke mipango madhubuti ya kuhakikisha shabiki anakua salama na hapatwi na kadhia katika jukumu lake la uchezaji wa kumi na mbili.


NB: Unaweza kwenda uwanjani na meno 32 ukarudi nyumbani na meno 28.

Sambaza....