Sasa Simba na Yanga zinapishana katika viwanja vya ndege vya Kimataifa wakienda kupambana na vigogo wengine Afrika, wakati pia tuna uhakika wakupata mechi nzuri kila weekend pale Kwa Mkapa
Usinga wa Yanga umerejea kwenye mkono wake wa kushoto, Namba tano imerejea kuwa eneo lake, uwanjani ni Ofisi yake na ‘First Eleven’ ya Yanga ni wafanyakazi wenzake na yeye akiwa Kingozi wao
Pia kwakumpanga Saidoo namba 10 halafu Chama winga moja na winga nyingine huanza Sakho, ambapo mara nyingi Chama huingia ndani na kumfanya Shomary Kapombe au Mohamed Hussein kupanda na kushambulia kwakutokea pembeni na hapa ndio tatizo lapili huonekana.