Ligi Kuu

Yacouba bora mwezi Februari!

Sambaza....

Nyota wa klabu ya Ihefu Yacouba Sogne ameibuka kinara katika tuzo za mwezi February yeye pamoja na kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime.

Yacouba Sogne aliejiunga na Ihefu katika usajili wa dirisha dogo ameibuka kinara baada ya kufunga mabao mawili mawili na kutoa pasi moja ya bao katika michezo miwili aliyoshuka dimbani na hivyo kuwashinda Meddier Kagere na Elius Maguri.

 

Yacouba Sogne ameoneoana kuanza kuimarika baada ya kupona majeraha ya goti yaliyomuweka nje mda mrefu sana na kupelekea Yanga kuamua kuachana nae. Lakini sasa nyota huyo wa zamani wa Yanga ameonekana kuwa mchezaji muhimu kwa “Mbogo maji”

Kwa upande wa makocha Mecky Mexime ameibuka kinara baada ya kuwashinda Nasradinne Nabi wa Yanga na Fikirini wa Coastal Union. Mecky ameshinda michezo miwili na sare moja katika michezo mitatu aliyoshuka dimbani mwezi wa pili.

Yacouba Sogne.

Pia kwa upande wa uwanja meneja wa uwanja wa Highland Estate Omary Malule kuwa meneja bora kwa mwezi husika.

Sambaza....