Shirikisho Afrika

Yanga: Tutaanza na siku ya Mashujaa halafu tutamaliza na paredi siku ya mchezo

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga imetoa ratiba yao ya wiki nzima kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir utakaopigwa siku ya Jumapili Bejamin Mkapa.

Ally Kamwe msemaji wa klabu ya Yanga amesema siku ya Ijumaa watakua katika hospitali ya Mloganzila ili kutoa damu na kuweza kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji.

 

Kamwe ameeita siku ya Ijumaa ni siku ya Mashujaa lakini pia hakusita kuyaalika makampuni mbalimbali ili waende pamoja katika siku hii muhimu kwa Wananchi.

“Tunakaribisha makampuni, taasisi na wadau mbalimbali watakaokua tayari kuwa na sisi katika siku ya mashujaa.

Tunatamani watu wanapotoka kutoa damu pale Mloganzila watoke na tiketi zao mkononi.
Makampuni tunatoa fursa hii idadi ni ileile minimum tiketi ni ileile 100 ukinunua utapata milage unayopaswa tutapost katika instagram yetu,” Alli Kamwe alisema

Alli Kamwe msemaji wa klabu ya Yanga.

Pia kuelekea katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho ambao ni muhimu kwa Yanga kushinda ili kupata nafasi yakwenda robo fainali Yanga wamesema wataandaa paredi ambayo itaanzia makao makuu ya klabu Jangwani mpaka uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa.

Alli Kamwe “Jumapili siku ya mchezo hii sasa ndo itakua kubwa kuliko, si mnajua Yanga hatunaga jambo dogo?. Tutaondoka hapa makao makuu Jangwani na paredi ya robo fainali.

Msafara utatoke hapa jeshi la polisi lipo tayari kutuongoza tutatoka hapa na king’ora mpaka uwanjani.”

Mashabiki wa klabu ya Yanga wakiwa ndani ya Dimba la Benjamin Mkapa.

Kamwe pia amewaita mashabiki na wanachama wote wanaotokea mkoani wakifika Jijini Dar wasipate tabu waende moja kwa moja Makao makuu ya klabu Jangwani.

“Wanachama na matawi yote yanayotoka mkoani wasipate tabu waje makao makuu tutaondoka wote kwenda uwanjani. Tunataka Waarabu waseme, waone watu wengi wanakuja hukoo,” alimalizia Alli Kamwe.

Yanga wanawakaribisha US Monastir katika uwanja wake wa nyumbani wakitaka kulipa kisasi baada ya mchezo wa awali kufungwa mabao mawili kwa sifuri Tunisia.

Sambaza....