Zahera
Blog

Yanga wanamvumilia Zahera kwa sababu ya Umasikini tu

Sambaza....

Nyakati kama hizi kipindi cha nyuma kwenye ligi kuu yetu kungekuwepo na joto kali sana la ubingwa. Hapana shaka huu ndiyo muda ambao timu za Simba na Yanga huwa zinawaza ubingwa tu.

Ndiyo muda ambao hesabu nyingi huwa zinapigwa ni namna gani ambavyo timu zao zinaweza kubeba ubingwa. Yani kwa kifupi hakuna neno ambalo huwa wanatamani kulisikia kipindi kama hiki kama ubingwa.

Ndipo hapo presha huwa kubwa sana kuanzia ndani ya klabu husika. Mazingira hutengenezwa ndani ya klabu husika ili tu kuongeza nguvu za ubingwa.

Ndiyo muda ambao klabu huangaika kutafuta pesa nyingi zaidi kwa ajili ya kuwekeza motisha ndani ya timu ili tu timu husika isitetereke kabisa kwenye mbio za ubingwa.

Hapa ndipo joto huwa linakuwa kubwa sana. Ukikuta timu inapoteza hata alama moja kelele huwa zinakuwa nyingi sana.

Presha huwa kubwa sana kwa wachezaji kutoka kwa mashabiki. Kocha huwa anakuwa anashinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu husika.

Na kuna uwezekano mkubwa sana kocha anaweza kupoteza kibarua chake kipindi hiki kama tu akipoteza alama ambazo zinaweza kuifanya moja ya hizo timu kutoka kwenye mbio za ubingwa.

Hiyo yote ilikuwa zamani. Zamani ambapo timu zote zilikuwa ni imara. Timu zote zilikuwa zinatamani kuwa mabingwa kutoka moyoni.

Lakini kwa sasa hilo halipo kabisa kwa sababu Yanga haiko kwenye nafasi kama hii ambayo tunaiongelea kwa sasa. Ipo kwenye nafasi ya kawaida sana.

Kwao wao kwa sasa kushinda kombe la ligi kuu ya Tanzania bara ni kitu ambacho hawakitegemei sana ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Ndiyo Yanga ilipofikia kwa sasa. Hata sehemu ambayo wapo kwa sasa hawaamini kama wapo , na hawaamini kama wataendelea kuwepo pale.

Wanajua wakati wowote wanaweza kabisa kutoka pale walipo kikubwa kinachosubiriwa ni suala la muda tu kwao wao kutoka pale kwenye uongozi wa ligi.

Hawaaamini kabisa kama wanaongoza ligi kwa sasa. Na haya yanaweza kuwa mafanikio makubwa sana kwao msimu huu ukilinganisha na uchumi ulivyo.

Yanga imefanikiwa sana msimu huu. Mafanikio ambayo hawaamini mpaka sasa kuwa wameyafikia mpaka muda huu.

Yanga imefanikiwa?. Najua ndilo swali ambalo unajiuliza mpaka sasa hivi na hupati jibu sahihi la swali lako ambalo linapita kichwani mwako.

Lakini huu ndiyo ukweli ambao hauna kificho mpaka sasa hivi Yanga imefanikiwa sana msimu huu ndiyo maana hawaamini sehemu waliyopo kwa sasa.

Niliwahi kubahatika kumsikia kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera akihojiwa na kituo kimoja cha Habari hapa nchini baada ya yeye kutoletewa wachezaji ambao aliwataka kwenye dirisha dogo la usajili.

Haruna moshi ndie mchezaji pekee aliesajiliwa na Mwinyi Zahera

Mwinyi Zahera alidai kuwa walielewana yeye na viongozi wa klabu ya Yanga kuwa mpaka mzunguko wa kwanza unamalizika timu iwe inashika nafasi ya tatu.

Hili ndilo lengo lao mama ambalo waliliweka wakati wanaanza ligi na wakati wamekaa na kocha wao kumwelezea malengo ya klabu kwa msimu huu.

Na katika kuelezana huko, Mwinyi Zahera alidai hicho kitu kinawezekana kabisa na kuwaomba viongozi wa Yanga kuwa kwenye dirisha dogo aletewe wachezaji ambao watamsaidia kumaliza ligi akiwa nafasi ya tatu.

Lakini mpaka sasa hivi Yanga iko nafasi ya kwanza. Ndiyo maana nakuambia Yanga imefanikiwa sana msimu huu na hawaamini kama mpaka sasa wamefanikiwa kiasi hicho.

Ndiyo maana hawana ile presha kubwa ya kupata ubingwa kama kipindi cha nyuma ilivyokuwa inakuwa kwenye klabu yao.

Ndiyo maana hata kama wakipoteza mechi kipindi hiki ambacho hawatakiwi kupoteza mechi ili wawe mabingwa wao hawana wasiwasi.

Hawaumii sana, kwa sababu wanajua hawawezi kuwa mabingwa, na nafasi waliyopo hawaamini kama wapo kwenye nafasi hiyo.

Mashabiki wa Yanga katila moja ya mechi za Ligi Kuu Bara

Kipindi cha nyuma kwenye vilabu hivi viwili, nyakati kama hiki kama timu ikipoteza hata alama moja na ikayumba kwenye mbio za ubingwa kelele zingepigwa sana.

Joto na presha ndani ya timu ingekuwa kubwa. Mashabiki wangesimama kudai ubingwa wao ambao wanaona kabisa unaondoka.

Lakini kwa sasa hii hadithi haipo tena kwa Yanga. Wanaamini matokeo yoyote ambayo wanaweza kuyapata kipindi hiki yanaakisi uwezo wa Yanga.

Uwezo wa Yanga kwa sasa kiuchumi ni mbovu, hawana uwezo wa kuifanya timu yao iwe imara kwa ajili ya kushindaniana ubingwa.

Hawana tena uwezo wa kutengeneza kikosi imara ambacho kinaweza kupigana kwa nguvu zote mwanzo hadi mwisho wa ligi.

Ndiyo maana kwao wao kwa kipindi hiki wanaona ni kawaida tu kufungwa kipindi hiki kwa sababu wanawachezaji ambao ni wakawaida.

Wachezaji ambao hawana uwezo mkubwa wa kubeba ligi kuu. Na hii ndiyo sababu kubwa hata kocha Mwinyi Zahera wanamvumilia. Ni kumuonea kumfukuza kwenye aina hii ya timu. Ila angekutana na Yanga yenye hali nzuri muda tungekuwa tunaongea Habari za kuondoka kwa Mwinyi Zahera.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x