Mabingwa Ulaya

Zlatan: Makombe yanamuogopa Mourinho

Sambaza....

Nyota mwenye maneno mengi ya jeuri na mbabe kwelikweli Zlatan Ibrahimovic amemwagia sifa Kocha Josse Mourinho na kusema ni moja ya Meneja aise muoga na mwenye desturi ya ushindi.

Zlatan Ibrahimovic: “Unataka kuwa mshindi popote uendako, basi ungana na meneja bora duniani Jose Mourinho. Yeye ni aina ya Meneja ambaye haogopi chochote. Yeye ni kama Zlatan. Haogopi bosi wa Klabu, Wacheza, Wanahabari. Kitu pekee anachokuwa akiogopa ni kutokupeleka Kikombe kwa Klabu yake.”

Jose Mourinho

Nyota huyo wa Sweden pia aligusia jinsi ambavyo Josse alivyomshawishi kwenda kujiunga na United ili kuendezeleza mipango ya kushinda makombe.

“Nilishinda (vikombe) naye huko Inter Milan, na nilipokuwa klabuni PSG alinipigia simu (Josse) na kusema “Hutaki kuja hapa Manchester United, ni msimu wangu wa kwanza hapa na kila mtu anaonekana kuwa wa kushangaza. Jezi, Beji inaonekana ni ya kushangaza kwa hivyo ikiwa utakuja kushinda tutawasaidia kushinda Kombe au Makombe, uwepo wako utawapa wachezaji hawa nguvu kubwa.

 

Nilisema kwanini sivyo. Nilipofika huko ilikuwa timu changa sana ambayo inacheza Ligi ya Europa. tutashinda, kwa sababu Nyara anamheshimu Zlatan na Jose Mourinho.”

Zlatan Ibrahimovic “Ibra Cadabra” anaonyesha jinsi mipango yao ilivyotimia kati yake na Josse Mourinho Manchester na baadae kuondoka na kuiacha klabu hiyo ikiendelea kuteseka na kushinda makombe.

Cadabra “Tulishinda makombe matatu au mawili mwaka huo na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa. Jose na mimi tuliachana na Klabu na walirudi nyuma bila kushinda chochote. Kwa hivyo lazima uangalie Tottenham msimu ujao kwani Jose ataanza msimu wake wa kwanza kamili nao.”

Sambaza....