Fiston Kalala Mayele ana mabao kumi na mbili katika Ligi Kuu ya NBC ambayo mpaka sasa imechezwa michezo 24. Wakati Rodgers Kola ana mabao nane akishika nafasi ya nne katika chati hiyo.
Kola wa Azam Fc yupo nyuma kwa mabao ya George Mpole (13), Fiston Mayele (12) na Reliant Lusajo (10), na jana katika mchezo dhidi ya Simba ndio alifunga bao lake la nane.
Kitu unachotakiwa kufahamu kuhusu Rodgers Kola aliesajiliwa msimu huu na Azam ni kwamba amewafunga Simba katika michezo yote miwili ya Ligi Kuu ya NBC na sio kwa bahati mbaya.
Mikimbio, kasi na kusimama katika eneo sahihi ndio kitu Kola alimzidi Mayele na kupelekea kufunga katika mechi zote mbili mbele ya Inonga na Onyango. Tazama hapa chini jinsi Tigana alivyomchambua Kola na kumtabiria goli katika mchezo wa jana.
Licha ya Fiston Mayele kuoneoana ni moja ya washambuliaji hatari na bora katika Ligi lakini hakufanikiwa kufunga bao lolote mbele ya walinzi bora Inonga Baka na Joash Onyango katika michezo yote miwili.