Sambaza....

Kuna sababu nyingi za msingi zinazonitaka
Aishi Manula asimame katika lango la Mnyama Simba katika pambano lao na Al Ahly, kesho ijumaa katika ufunguzi wa African Football League.

Nafahamu Manula ametoka katika chumba cha majeraha na hana utimamu wa kisawasawa, lakini nakupa sababu tatu za msingi za kwanini anatakiwa kucheza mechi hiyo.

Aishi Manula akiwa mazoezini na Simba baada ya kupona majeraha yake.

UZOEFU

Hili ni eneo ambalo Manula amewaacha wenzake kwa umbali mrefu. Manula amecheza mechi nyingi kubwa zenye sura ya namna hii, hivyo uwepo wake utakuwa na faida kubwa katika lango la Mnyama.

UIMARA

Bado Simba SC hawajampata kipa namba moja tangu Manula aumie katika pambano la Ihefu msimu uliopita pale Chamazi.

Sio Ayub, sio Ally wala Hussein waliokata kiu ya mashabiki wa Simba SC tangu Manula yuko nje mpaka sasa amerejea kwenye nafasi yake.

Ally Salim akiokoa mkwaju wa penati wa penati katika katika mchezo wa Ngao ya hisani dhidi ya Singida Fountaine Gate Fc.

Kama Ally, Ayoub na Hussein wangelishika kisawasawa lango la Simba SC, kusinhekuwa na minong’ono ya watu kutaka Manula arejee haraka kiwanjani.

IMANI

Imani ni jambo kubwa katika mambo mengi. Manula anaaminiwa, hii inampa nafasi ya yeye kufanya vyema ili kutotaka kuwaangusha wale waliomuamini. Hii peke yake inatosha kumpa nafasi ya kucheza Manula katika mechi ya Ijumaa.

Imani anayopata Manula ni kutokana na yeye kuwahi kuwaaminisha kuwa anaweza. Hivyo jambo la imani ni jambo linalompa nafasi ya kucheza.

Sambaza....